“Let each thing you would do, say or intend be like that of a dying person.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 2.11.1

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ADHABU YAKO YA KIFO…
Siku uliyozaliwa, ndiyo siku hiyo hiyo ambayo ulipewa adhabu kuu ya maisha yako, adhabu ya kifo.
Hivyo kila sekunde ya maisha yako inayopita, unajisogeza karibu zaidi na adhabu yako ya kifo.
Hakuna awezaye kuikwepa adhabu hii, hata awe mfalme anayetukuzwa na kila mtu, wakati wake utafika wa kuitumikia adhabu yake.

Tunakumbushana hili siyo kwa ajili ya kutishana au ili kuponda raha na kula maisha, bali kufikiria kabla ya kusema au kufanya chochote.
Kutokuruhusu tupoteze muda wetu kwenye vitu visivyo na msingi.
Kuacha kuahirisha mambo kama vile utaishi milele.
Kuacha kuhangaika na mambo yasiyo na mchango wowote kwako au kwa wengine.
Kwa sababu muda ulionao unahesabika, ni vyema kuutumia kwa yale muhimu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuikumbuka adhabu yako ya kifo na kutambua kwamba kila sekunde inayopita unajisogeza karibu zaidi na adhabu yako. Hivyo weka vipaumbele vyako vizuri ili ufanye yaliyo muhimu.
#KifoNiAdhabuYaKilaMtu #UsiogopeKifoOgopaKutokuishi #JikumbusheUkomoWaMudaWako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania