“Philosophy does not claim to get a person any external possession. To do so would be beyond its field. As wood is to the carpenter, bronze to the sculptor, so our own lives are the proper material in the art of living.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.15.2

Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MSANII WA MAISHA NA KIFO.
Mwanafalsafa ni msanii wa maisha na kifo.
Hii ni kwa sababu lengo kuu la falsafa ni kujifunza jinsi ya kuishi vyema.
Na ukiweza kuishi vyema basi hutakuwa na wasiwasi wala kuhofia kifo.
Kwa lengo hili kuu la falsafa, kila mtu anaihitaji falsafa, kila mtu anaweza kunufaika nayo.
Falsafa siyo kwa ajili ya wanataaluma au matajiri wachache,
Bali ni sanaa ambayo iko wazi kwa kila mtu na yeyote anaweza kunufaika nayo.

Wewe ni msanii wa maisha na kifo,
Na falsafa ndiyo nyenzo yako kuu kwenye sanaa hii, kama ilivyo kalamu kwa mwandishi, kipaza kwa mwimbaji au koleo kwa mchongaji.
Imarisha na kutumia nyenzo hii muhumu kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi kila siku.
Na ukiweza kuishi vizuri, basi huna haja ya kuhofia kifo. Maana hakuna chochote utakachobakisha kwenye kila siku yako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuiishi falsafa kama mwongozo mkuu kwako kuwa na maisha bora. Siku ya kuchagua kuwa msanii wa maisha yako.
#MaishaNiSanaa #FalsafaNiNyenzoKuu #IshiKilaSikuYako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania