“Keep death and exile before your eyes each day, along with everything that seems terrible—by doing so, you’ll never have a base thought nor will you have excessive desire.”
—EPICTETUS, ENCHIRIDION, 21
Ni jambo la kushukuru sana kwa sisi kuweza kuiona siku hii mpya na nzuri sana ya leo.
Siyo kwa nguvu zetu wala akili zetu, ila ni kwa bahati tu.
Tunapaswa kuitumia siku hii vyema ili kuweza kupiga hatua zaidi.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USILOTEGEMEA LAWEZA KUTOKEA…
Huwa tunaweka mipango yetu mbalimbali,
Tukiwa tunajua kabisa ni nini tunachotaka kupata kwa kile tunachofanya.
Na hapo tunakuwa tunategemea kile tunachotaka ndiyo kitokee.
Lakini kwenye unalisia hivyo sivyo mambo yanavyokwenda.
Usiyotegemea ndiyo huwa yana nafasi kubwa ya kutokea na haya huwakuta wengi wakiwa hawana maandalizi.
Usikubali kuendelea kushangazwa na matokeo ya tofauti unayokutana nayo.
Badala yake kwenye kila mpango unaojiwekea, jua kabisa yale usiyotegemea yatokee yanaweza kutokea, tena yana mafasi kubwa ya kutokea kuliko yale unayotegeme yatokee.
Hivyo mara zote kuwa na maandalizi iwapo yale usiyotegemea yatokee yatatokea na hilo halitaweza kukukwamisha.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutegemea yale usiyopenda yatokee kutokea na hivyo kuwa na maadalizi sahihi ya kukabiliana nayo.
#UsiyoyapendaYatatokea #KuwaNaMaandalizi #ChukuaHatuaSahihi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania