“Don’t behave as if you are destined to live forever. What’s fated hangs over you. As long as you live and while you can, become good now.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.17

Kuiona siku hii mpya ya leo ni jambo la kipekee sana kwetu.
Siyo kila aliyepanga kuiona leo amepata bahati hii,
Lakini sisi tumebahatika, tunapaswa kuitumia nafasi hii vyema.
Kwa kwenda kuweka juhudi kwenye kila tunachofanya ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MUDA WA KUWA MWEMA NI SASA…
Ni rahisi kujiambia kwamba una muda wa kurekebisha makosa unayoyafanya sasa.
Lakini je unajua muda ulionao ni kiasi gani?
Vipi kama ulionao sasa ndiyo muda wako wa mwisho na hivyo huwezi kupata nafasi nyingine ya kurekebisha makosa unayoyafanya?

Rafiki, muda pekee ambao una uhakika nao kwenye maisha yako ni sasa, na hivyo huu ndiyo muda mzuri kwako kuwa mwema.
Usijifanye kama vile utaishi milele, usijipangie mambo yako kwa muda ujao, ambap huna uhakika nao.
Ishi vizuri sasa, tenda wema sasa na kama itakuwa mwisho, utakuwa umeyaishi maisha yako vyema.
Na kama utapata nafasi nyingine, basi ni fursa ya kuishi vyema pia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa mwema kwa wakati ulionao na kufanya kilicho sahihi sasa, kwa sababu huenda usipate nafasi nyingine kama uliyonayo sasa.
#KuwaMwemaSasa #HutaishiMilele #TumiaVizuriMudaUlionao

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania