“I say, let no one rob me of a single day who isn’t going to make a full return on the loss.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 1.11b
Hongera mwanamafanikio kwa kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USIJIUZE KWA BEI RAHISI…
Kitu chochote unachofanya na muda wako, jua unauza muda wako.
Sasa kama ilivyo kwa vitu vingine tunavyouza, huwa tunahakikisha tunapata thamani halisi, hatupendi kuuza vitu vyetu kwa bei rahisi.
Lakini inapokuja kwenye muda wetu, inapokuja kwenye maisha yetu, tupo tayari kuuza muda wetu hata bure kabisa.
Unapotumia muda wako kufanya mambo ambayo hayana mchango mkubwa kwako umechagua kuuza muda wako kwa bei rahisi.
Unapotumia muda wako kifuatilia maisha ua wengine, kubishana, kufuatilia habari, jua unauza muda wako kwa bei rahisi.
Kwa sababu muda unapotoka haurudi tena, hivyo kama hakuna cha maana ulichopata, umechagua kupoteza muda wako.
Linda sana muda wako, pima kila unachotaka kufanya kabla hujaanza kufanya. Jiulize je hapa najiuza kwa bei rahisi au bei ghali?
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kulinda muda wako na kuacha kuupoteza kwa mambo yasiyo na mchango kwako.
#UsijiuzeKwaBeiRahisi #ThaminiMudaWako #TafakariKablaYaKufanya
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania