“Soon you will die, and still you aren’t sincere, undisturbed, or free from suspicion that external things can harm you, nor are you gracious to all, knowing that wisdom and acting justly are one and the same.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.37

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine mpya tuliyoiona leo.
Ni fursa ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HEKIMA NA HAKI…
Kuna misingi mingi muhimu kwenye maisha, lakini kuna hii miwili muhimu mno, ambayo ukiijua na kuiishi kila siku, utakuwa na maisha bora sana.
Misingi hiyo miwiki ni HEKIMA ya kujua unaweza kufa leo na kutenda kwa HAKI kila wakati.
Misingi hii miwili inabeba misingi mingine yote kama mtu utaweza kuiishi vizuri.

Misingi hii inatokana na ukweli wa maisha kwamba kila mtu atakufa na njia pekee ya kuyaishi maisha yako ni kufanya kile kilicho sahihi.
Hivyo kama utakubali na kuelewa hayo, na kisha kuyaishi kila siku, kila siku itakuwa bora sana kwako.
Unapokubali kwamba unaweza kufa leo, huwezi kuahurisha yale muhimu kwako kufanya na hivyo unaweka vipaumbele vyako vizuri.
Unapotenda kwa haki, unakuwa umefanya kilicho sahihi na hivyo huna haja ya kujiuliza wengine wanakuchukukiaje.
HEKIMA NA HAKI vitakufanya kuwa huru na maisha yako ya kila siku.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukubali unaweza kuwa ndiyo mwisho wako na hivyo kutenda kila kitu kwa haki.
#MudaWakoUnahesabika #MaraZoteFanyaKilichoSahihi #UsiahirisheYaliyoMuhimu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania