“I tell you, you only have to learn to live like the healthy person does . . . living with complete confidence. What confidence? The only one worth holding, in what is trustworthy, unhindered, and can’t be taken away—your own reasoned choice.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.26.23b–24
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana kwetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KITU PEKEE UNACHOWEZA KUKIAMINI NA KUKITEGEMEA KWENYE MAISHA YAKO…
Ni fikra zako.
Hiki ndiyo kitu pekee ambacho hakuna anayeweza kukunyang’anya,
Ndiyo kitu pekee ambacho uko huru nacho, hata ukifungwa, bado hakuna awezaye kufunga fikra zako.
Hivyo ukiamini na kutegemea fikra zako, muda wote unakuwa huru bila ya kujali nini kinaendelea kwenye maisha yako.
Vitu vingine vyote unaweza kuvipoteza haraka kwenye maisha yako,
Wengine wanaweza kuchukua katibu kila kitu kwenye maisha yako,
Lakini fikra zako, hakuna aliye na nguvu nazo isipokuwa wewe peke yako.
Tambua nguvu hii ya kipekee iliyopo kwenye fikra zako na itumie ikusaidie kuwa na maisha bora, tulivu na yenye mafanikio makubwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutambua kwamba fikra zako ndiyo kitu pekee unachoweza kukiamini na kukitegemea kwenye maisha yako.
#UhuruUpoKwenyeFikra #FikiriKwaUsahihi #LindaFikraZako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania