Ni kwa sababu hujui kwa hakika nini unachotaka.
Na kama unajua, basi hujajitoa kweli kuhakikisha kwamba unakipata.
Ndiyo maana kila fursa mpya inayojitokeza inakuyumbisha.
Ndiyo sababu kila mwaka unajaribu biashara mpya, ukikutana na ugumu unaacha na kwenda kujaribu biashara nyingine.
Kanuni ya kwanza ya kupata unachotaka ni kujua kwanza kile halisi unachotaka, halafu kujitoa kuhakikisha unakipata bila ya kuruhusu kitu chochote kikuzuie.
Haya ni maamuzi ambayo wengi hawayafanyi zama hizi, na hilo limetokana na wingi wa fursa zilizopo sasa na ukosefu wa subira kwa walio wengi. Watu wanataka kitu na wanakitaka sasa, hawataki kusubiri.
Hakuna mafanikio makubwa yanayokuja kwa haraka, hayapo, na hata yakitokea basi huwa hayadumu. Mafanikio ya kudumu yanajijenga kwenye msingi imara, ambao unachukua muda.
Usikubali kuendelea kuwa mtu wa kuzurura hapa duniani, kujaribu kila kinachopita mbele yako. Amua ni nini unataka, wapi unakwenda au kutaka kufika na kisha weka juhudi zako zote kuhakikisha unafika huko, bila ya kuruhusu chochote kuwa kikwazo kwako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Shukrani kocha Kwa makala hii nzuri kwangu.
Nimejifunza na kukumbushwa kitu Muhimu hapa. Asante.
LikeLike
Vizuri Tumain.
LikeLike