“Death lies heavy upon one
who, known exceedingly well by all,
dies unknown to himself.”
—SENECA, THYESTES, 40

Tumeiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Siku mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tunakwenda kuiishi siku hii kwa kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JITAMBUE KABLA HUJACHELEWA…
Watu wengi wamekuwa wanaishi maisha yao hapa duniani, mpaka wanakufa bila ya kujitambua na kujijua vizuri wao wenyewe.
Wengine wanaweza kuwajua kiundani lakini wao wenyewe wakawa hawajijui.
Hii ni hasara kubwa sana kwa sababu kama hujajitambua hujayaishi maisha yako.
Chochote unachofanya kabla hujajitambua ni maigizo tu, siyo uhalisia wako.

Hivyo kabla hujaendelea na mbio zako za maisha, kabla hujaendelea na safari usiyoielewa, ni vyema kutenga muda na kuchimba ndani yako ili kujitambua wewe mwenyewe.
Ni muhimu ujijue kwa undani, unapenda nini, hupendi nini, una uimara gani na udhaifu gani, unajali nini zaidi, una kipaji na kusudi gani na alama gani unataka kuiacha hapa duniani.

Ukishajitambua, maisha yako yote yanabadilika, hutapoteza tena muda, hutakuwa tena mtu wa kuahirisha mambo na hutasubiri mpaka usukumwe ndiyo ufanye unachotaka kufanya.
Usikubali kuendelea na maisha ya maigizo, hakikisha unajitambua wewe mwenyewe kwanza, ili uweze kuendesha maisha halisi kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujitambua wewe mwenyewe na kuishi maisha halisi kwako na siyo maigizo.
#Jitambue #IshiMaishaYako #UsiigizeMaisha

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania