“Do you then ponder how the supreme of human evils, the surest mark of the base and cowardly, is not death, but the fear of death? I urge you to discipline yourself against such fear, direct all your thinking, exercises, and reading this way—and you will know the only path to human freedom.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.26.38–39
Kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo ni bahati kubwa kwetu.
Wapo wengi waliopanga kuiona siku hii lakini hawajapata mafasi ambayo sisi tumeipata.
Na siyo kwamba tunastahili sana, bali ni kwamba kazi yetu bado haijakamilika.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KITU PEKEE UNACHOPASWA KUHOFIA…
Kitu pekee unachopaswa kuhofia kwenye maisha yako ni hofu ya kifo.
Hupaswi kuhofia kifo, kwa sababu hakuna namna utakikwepa,
Bali unapaswa kuhofia hofu ya kifo, maana hii ndiyo inayokunyima wewe utulivu wa moyo.
Hii ndiyo inaondoa kwako msukumo wa kupiga hatua zaidi,
Hii inakufanya ushindwe kuyafurahia maisha yako sasa.
Ndiyo utakufa, lakini kupoteza muda wako kila siku kujiuliza utakufaje na nini kitatokea utakapokuwa, ni matumizi mabaya ya muda na akili yako.
Kila wakati kuwa tayari kwa ajili ya kifo, lakini usipoteze hata dakika moja kukihofia kifo hicho.
Kwa sababu haijalishi unakihofia kiasi gani, hakubadilishi chochote, hakutakisogeza mbele au kupunguza makali yake.
Ishi maisha yako leo kwa ukamilifu, ishi kama ndiyo siku ya mwisho na usikubali hofu ya kifo ikutawale na kukuzuia kuyafurahia maisha uliyonayo leo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutoruhusu hofu ya kifo ikutawale na kukunyima kuwa na maisha huru.
#HupaswiKuhofiaKifo #KuishiVizuriNiKujiandaaKufa #HakunaAtakayetokaHapaHai
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.t.me/somavitabutanzania