“You know what wine and liqueur tastes like. It makes no difference whether a hundred or a thousand bottles pass through your bladder—you are nothing more than a filter.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 77.16
Ni jambo la kushukuru sana kwetu sisi kuiona siku hii mpya ya leo.
Siyo kwa nguvu zetu au akili zetu, bali ni kwa bahati pekee.
Hivyo ni wajibu wetu kushukuru na kuitumia siku hii vyema ili iwe na maana kwetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari VITU VINGI HAVINA MAANA AMBAZO UNAVIPA…
Kuna vitu ambavyo tunavitukuza sana kwenye maisha yetu, tunavipa maana kubwa, tunakuwa tayari kulipa fedha nyingi kuwa navyo.
Lakini vitu hivyo havina maana wala thamani ambayo tunavipa.
Tunakuwa tunajisumbua tu na kuhangaika, lakini hakuna maana yoyote.
Mfano wa vitu vinavyotusumbua na visivyo na maana ni vyakula, mvinyo, mavazi, umaarufu na hata wengine wanavyotuchukulia.
Watu huwa tayari kulipa kiasi kikubwa ili kupata mvinyo ambao umekaa muda mrefu na hivyo kuiva na kukomaa zaidi.
Lakini unafikiri mvinyo huo unaleta tofauti gani kwenye mwili wako?
Mwisho wa siku utaishia kuchujwa kwenue figo na kutolewa kama uchafu kupitia mkojo.
Hivyo kitu ambacho umehangaika nacho sana, unaishia kwenda kukimwaga chooni.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa vitu vingine, aliyekula kuku na aliyekula maharage wote wamepata protini na mwisho wa siku mabaki yake yanaenda chooni.
Tafakari hii inatusaidia kuvipa vitu maana na thamani sahihi na kutosumbuka na maana zisizo sahihi.
Kwa kuvipa vitu maana na thamani sahihi kunakupa utulivu mkubwa na kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuvipa vitu maana na thamani sahihi na kutoruhusu kitu chochote kile kikusumbue.
#VituVingiVinapita #UsisumbukeNaChochote #HakunaKilichoMuhimuKulikoWewe
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Ahsante sana kocha umenifanya nitafakari sana juu ya thamani ya tunayoipa vitu
Tunathaminisha vitu vingi sana kuliko uhalisia haswa pale tunapokuwa hatujavipata
Hisia zikishatukamata tunafanya maamuz mabovu sana na ukija kukaa na kufikiri hvyo vitu havikuwa na thamani halisi kama tunayoipa n kujilisha upepo tu!!!
LikeLike
Karibu Hendry.
LikeLike