“It’s not at all that we have too short a time to live, but that we squander a great deal of it. Life is long enough, and it’s given in sufficient measure to do many great things if we spend it well. But when it’s poured down the drain of luxury and neglect, when it’s employed to no good end, we’re finally driven to see that it has passed by before we even recognized it passing. And so it is—we don’t receive a short life, we make it so.”
—SENECA, ON THE BREVITY OF LIFE, 1.3–4a

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA NI MAREFU KAMA UNAJUA JINSI YA KUYATUMIA…
Kila mtu analalamika maisha ni mafupi na hana muda.
Inapokuja kwenye kufanya mambo muhimu kwa mtu kupiga hatua, kama kujifunza kupitia usomaji wa vitabu, kuanzisha biashara ukiwa kwenye ajira au kuboresha mahusiano yako na wengine, wengi wamekuwa wanatoa sababu kwamba hawana muda wa kufanya hivyo.

Lakini ukipewa nafasi ya kuyaangalia masaa 24 ya siku ya mtu yeyote yule, utashangaa jinsi ambavyo anapoteza muda wake.
Mtu huyu anayelalamika maisha ni mafupi na hana muda, utamkuta akifanya yafuatayo;
👉🏼Anatumia mitandao ya kijamii na kila siku lazima apite kwenye mitandao hiyo kuona nini kinaendelea.
👉🏼Anafuatilia habari mbalimbali zinazoendelea.
👉🏼Anafuatilia michezo anayoipenda.
👉🏼Anapata muda na nafasi ya kubishana na watu wengine kwa mambo mbalimbali.
👉🏼Anakaa kwenye foleni kwa wastani wa masaa 2 kwa siku, hayo ni masaa zaidi ya 40 kwa mwezi, sawa na wiki moja ya kazi.
Na mengine mengi.

Hivyo unaweza kuona mwenyewe rafiki, kwamba tunachokosa siyo muda, bali tunautumia muda tulionao vibaya.
Kuanzia leo, kabla hujasema huna muda, kabla hujalalamika maisha ni mafupi, hebu kaa chini na orodhesha mambo yote uliyofanya kwa juma moja lililopita, na wewe mwenyewe utaona ni jinsi gani unapoteza muda wako mwingi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia vizuri muda ulionao ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#UnaMudaWaKutosha #UmekosaVipaumbele #UnahangaikaNaMamboMengi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania