“In all things we should try to make ourselves be as grateful as possible. For gratitude is a good thing for ourselves, in a manner in which justice, commonly held to belong to others, is not. Gratitude pays itself back in large measure.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 81.19

Kuiona siku hii nyingine mpya ya leo ni bahati kubwa sana kwetu,
Hatujaiona siku hii kwa nguvu zetu, wala akili zetu,
Bali ni kwa neema tu, kwa sababu bado kazi yetu hapa duniani haijamalizika.
Hivyo tunapaswa kuutumia muda wa leo vizuri, tufanyie kazi vipaumbele vyetu na tuweze kufanya makubwa.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TOA SHUKRANI…
Unapaswa kushukuru kwa kila jambo, liwe kubwa au dogo, zuri au baya, toa shukrani.
Unaposhukuru kwa jambo lolote lile, unaona upande chanya wa jambo hilo na kuona hatua sahihi za kuchukua.
Lakini unapokosa shukrani, unapokuwa mtu wa kulalamika na kulaumu kwa kila jambo, unaona upande hasi wa jambo na linakuwa gumu zaidi.

Kila unapoianza siku yako, anza kwa kuoridhesha vitu vitano mpaka kumi ambavyo unashukuru kuwa navyo kwenye maisha yako.
👉🏼Anza kwa kushukuru kwa uhai ulionao, ukijua wengi walipanga kuiona siku ambayo wewe umeiona lakini haijawezekana.
👉🏼Shukuru kwa mwenza uliyenaye, ambaye anakupenda kwa namna ulivyo, pamoja na mapungufu yote uliyonayo.
👉🏼Shukuru kwa familia uliyonayo, ambayo inakupenda na kukujali, ambayo ipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako.
👉🏼Shukuru kwa kazi au biashara uliyonayo inayokuingizia kipato cha kuendesha maisha yako, ukijua kuna wengi ambao hawana kipato kama chako.
👉🏼Shukuru kwa wakati huu unaoishi, wakati wa amani, wakati wa maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo yanarahisisha sana maisha, ukijua kuna watu waliishi nyakati ngumu, za vita na majanga mengine.

Unapoangalia, kuna mengi sana ya kushukuru kwenye maisha yako, bila ya kujali unapitia hali gani.
Na unapoanza kushukuru, unaona mengi zaidi ya kuendelea kushukuru kwenye maisha yako.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kushukuru kwa kila ulichonacho au unachopitia kwenye maisha yako.
#ShukuruKwaKilaJambo #UsilalamikeWalaKulaumu #OnaUpandeChanyaWaJambo

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania