At the heart of all religions lies a single unifying truth. Let Persians bear their taovids, Jews wear their caps, Christians bear their cross, Muslims bear their sickle moon, but we have to remember that these are all only outer signs. The general essence of all religions is love to your neighbor, and that this is requested by Manuf, Zoroaster, Buddha, Moses, Socrates, Jesus, Saint Paul, and Mohammed alike. —EWALD FLÜGEL
Zipo dini mbalimbali hapa duniani ambazo zina alama tofauti zinazozitambulisha.
Wakristo wanatambulika kwa alama ya msalaba,
Waislamu wanatambulika kwa alama ya mwezi,
Wayahudi wanatambulika kwa alama ya kofia,
Lakini alama hizi za nje hazina maana kubwa kwenye dini hizo.
Msingi wa dini zote ni upendo, kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.
Na hilo ndilo agizo la Muda, Yesu, Mohamad, Socrates na wengineo.
Dini ya kweli ni upendo,
Kama unataka kuienzi kweli dini yako au imani uliyonayo, basi anza na upendo kwako na kwa wale wanaokuzunguka.
Kusema kwamba wewe ni mtu wa dini au wa imani huku huna upendo kwako na kwa wengine ni kujidanganya mwenyewe.
Maana wengine wanaweza kukuona kwa nje ukikazana na alama za dini yako, lakini ndani yako utajua kabisa kwamba una unafiki.
Mwaka 2020 ukawe mwaka wa kuongozwa kwa upendo mkubwa,
Tuishi kwa upendo na kila tunalofanya tulifanye kwa upendo mkubwa kwetu na kwa wengine pia.
Kwa sababu upendo una nguvu kubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania