“Put at least half of your energy into making yourself free of empty wishes, and very soon you will see that in so doing you will receive much greater fulfillment and happiness.” —After EPICTETUS

Kinachofanya tusiyafurahie maisha yetu ni matumaini hewa ambayo tumekuwa tunajipa.
Unakuta umejiweka lengo la kupata kitu fulani, ukishakipata unakifurahia kwa muda mfupi, baadaye unajiambia ukipata cha juu zaidi ndiyo utafurahi.
Unakazana na unakipata, na furaha yako haidumu muda, unaona tena cha juu zaidi ambacho unajiambia ukikipata utafurahia maisha.

Haya ni matumaini hewa ambayo yanakuzuia usiyafurahie maisha yako na yasiwe bora.
Kuwa na maisha bora na unayoyafurahia, anza kuvunja matumaini hewa, anza kuweka nguvu zako kwenye kile unachofanya na kile ulichonacho sasa na siyo kile unachotamani kupata.
Kwa sababu hakuna wakati utapata kitu na kuridhika nacho kabisa, lazima kutakuwa na cha juu zaidi.

Unapoimaliza siku hii, tafakari ni namna gani umekuwa unaahirisha kuyaishi maisha yako kwa sababu ya vitu fulani unavyojiambia ni mpaka uwe navyo.
Kuanzia leo, amua kuyafurahia maisha uliyonayo na kile ulichonacho, na utashangaa jinsi ambavyo utaweza kupata zaidi na kupiga hatua zaidi.

Tuwe na usiku mwema.
Kocha.