Buddha said, “A man who starts to live for his soul is like a man who brings a lantern into a dark house. The darkness disappears at once. You have to be persistent in this, and your soul will have this light.”
Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri uliyoiona leo.
Una fursa kubwa mbele yako ya kwenda kuchukua hatua za tofauti ili kupata matokeo ya tofauti.
Unapochagua kuyaishi maisha yako, ni sawa na kupeleka taa kwenye chumba chenye giza, giza hilo hupotea mara moja.
Unapoyaishi maisha yako, unakuwa mwanga ambao unaangaza maisha ya wengine.
Wengine wanajifunza na kupata matumaini kupitia wewe, kwa kuchagua kuyaishi maisha yako na kuwa na msimamo wako.
Lakini unaposhindwa kuyaishi maisha yako, unapochagua kuyaishi maisha ya wengine, unaleta giza kwenye maisha ya wengine, kwa sababu hakuna cha tofauti wanachokiona kwako.
Unapaswa kuyaishi maisha yako, siyo tu kwa manufaa yako, bali pia kwa nuru utakayotoa kwa ajili ya wengine.
Na hili siyo rahisi, hivyo litakutana kujisukuma kuliko ulivyozoea.
Usikubali leo kuwa giza kwenye maisha ya wengine, chagua kuwa nuru, chagua kuangaza maisha ya wengine, chagua kuyaishi maisha yako, kwa sababu ndiyo maisha pekee uliyonayo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania