Christ expressed all His teachings in His last commandment: “Love each other, as I loved you. Everyone will see that you are my disciples, if you love each other.” He did not say, “If you believe,” but “If you love.” Faith can change with time, because our knowledge is constantly changing. Love, on the contrary, never changes; love is eternal.
Yesu alihitimisha mafunzo yake kwa wanafunzi wake akiwaambia, “pendaneni kama mimi nilivyowapenda na watu watajua kuwa ni wanafunzi wangu kupitia upendo wenu.”
Upendo ndiyo amri kuu, upendo ndiyo dini ya kweli.
Yesu hakuwaambia wanafunzi wake wakiamini ndiyo watakuwa wanafunzi bora, bali wakipendana.
Na hii ni kwa sababu imani inaweza kubadilika kadiri mtu anavyopata taarifa na maarifa, lakini upendo ni wa kudumu.
Hebu na sisi tukaishi kwa amri hii kuu, ambayo ndiyo dini ya kweli, ambayo ni UPENDO.
Haijalishi wewe ni Mkristo, Muislamu, Mbudha au usiye na dini, upendo una nguvu kubwa sana kwako, ya kukuwezesha kuwa na maisha bora.
Upendo uko wazi, upendo hauna unafiki.
Unapoimaliza siku ya leo jiulize je umeishi kwa upendo?
Je umejipenda wewe mwenyewe, kuwapenda wanaokuzunguka na kupenda unachofanya?
Kama kuna eneo lolote katika hayo matatu ambalo unakosa upendo, litaondoa utulivu kwenye maisha yako.
Wanasema kama hujapata unachopenda, basi penda ulichopata.
Popote ulipo, upendo utawale.
Nawapenda sana wote, na muwe na usiku mwema.
Kocha.