“Only when we forget what we were taught do we start to have real knowledge.” —HENRY DAVID THOREAU
Ni jambo kubwa sana na la kushukuru sisi kuweza kuiona siku hii nyingine mpya ya leo.
Tukiweza kuitumia vizuri, tutaweza kufanya makubwa sana leo.
Maarifa ya kweli yanaanza pale unaposahau kile ulichofundishwa au ulichosoma.
Hapo ndipo akili yako inapofanya kazi ya kufikiri na kisha kuja na namna sahihi ya kuchukua hatua kwenye jambo lolote lile.
Chochote unachofundishwa na wengine au kujifunza kupitia usomaji siyo zao la akili yako, bali ni kitu umebeba kutoka kwa wengine.
Mara nyingi vitu unavyobeba kutoka kwa wengine huwa vina ugumu wa kuvitumia kwenye maisha yako.
Hivyo ili kunufaika na unachofundishwa, ili kuweza kutumia vizuri maarifa unayopata na kupiga hatua, lazima utumie akili yako sawasawa.
Lazima ufikiri kwa kina kwa kila unachojifunza na jinsi unavyoweza kukitumia kwenye maisha yako.
Kwa sababu chochote unachojifunza ni namna ambavyo wengine wametumia kwenye maisha yao, ambayo ni tofauti kabisa na maisha yako.
Hivyo unapofikiri ndiyo unaweza kutumia vizuri maarifa unayoyapata.
Ni muhimu uihusishe na kuishughulisha akili yako kwenye yake unayojifunza, ili uweze kuyatumia na yalete matokeo ya tofauti kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania