“Knowledge is real knowledge only when it is acquired by the efforts of your intellect, not by memory.” – Leo Tolstoy

Maarifa bora kwako ni yale unayoyapata kwa kutumia akili yako kufikiri na siyo kwa kukariri.
Kwa kukariri unaweza kujua mengi, lakini usiweze kuyatumia.
Kwa kufikiri unaelewa vizuri ulichojifunza na jinsi unavyoweza kukitumia kupiga hatua zaidi.

Hivyo tumia akili yako sawasawa, siyo kwa kukariri visivyo na umuhimu, bali kwa kufikiri kwa usahihi na kupata majibu sahihi ya chochote unachopitia.

Unapoimaliza siku hii ya leo jiulize leo umetumia akili yako kufikiri au kukariri,
Je umefikiri kile unachofanya au umekifanya kama ulivyofanya jana?
Akili zetu zina uwezo mkubwa sana, kama tutazitumia vizuri.
Shughulisha akili yako na itakuwa msaada kwako.

Ukawe na wakati mwema,
Kocha.