“As we bring up our children, we have to remember that we are caretakers of the future. By improving their education, we improve the future of mankind, the future of this world.” —After IMMANUEL KANT
Ni jambo kubwa na la kushukuru sana kwa sisi kuweza kuiona siku hii nyingine nzuri ya leo.
Tukaitumie siku hii vyema ili tuweze kufanya makubwa na kupata matokeo bora.
Tumepewa jukumu kubwa sana la kuitengeneza kesho ya jamii ya wanadamu kupitia malezi ya watoto wetu.
Tunavyowalea watoto wetu ndivyo tunavyoitengeneza kesho ya wanadamu hapa duniani.
Hivyo tukiboresha elimu tunayowapa watoto wetu na kuwalea katika misingi sahihi, jamii ijayo itakuwa bora sana.
Lakini kama tutashindwa kuwalea kwenye misingi sahihi na tukashindwa kuwapatia elimu yenye manufaa kwao, sisi tutakuwa tumechangia kuharibu kesho ya jamii nzima ya wanadamu.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha anatumia kila nafasi aliyonayo kuboresha kesho ya jamii yetu.
Kwa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na kuijua misingi sahihi ya maisha ya mafanikio.
Tusikimbilie tu kuwapa watoto vitu rahisi na wanavyofurahia, bali tuwape vitu sahihi na vinavyowajenga kwenye maisha yao ya leo na ya baadaye.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania