“A man should use that spiritual heritage which he has received from the wise and holy people of the past, but he should test everything with his intellect, accepting certain things and rejecting others.” – Leo Tolstoy
Hoji na dadisi kila kitu kabla ya kukikubali na kukitumia.
Usiwe tu mtu wa kupokea na kukubali kila unachoambiwa,
Badala yake tumia akili yako kufikiri kwa usahihi, kuhoji na kudadisi ili uweze kupata uelewa sahihi na hapo unaweza kukubali au kukataa.
Usijisikie vibaya kukataa kitu hata kama kinakubalika na kila mtu.
Usijidharau na kuona kama wengine wamekubali wewe ni nani ukatae.
Una akili, hivyo itumie vizuri kwa manufaa yako.
Maana ukweli kuhusu wewe upo ndani yako na ni wewe pekee unayeweza kuujua.
Hoji na dadisi kila kitu kabla hujakubaliana nacho.
Tuwe na wakati mwema na maandalizi mazuri ya kesho yetu na jima jipya tunalokwenda kuanza.
Kocha.