“Faith is the understanding of the meaning of life and the acceptance of those duties and responsibilities connected to it.” – Leo Tolstoy,

Imani ni kujua maana na kusudi la maisha yako na kisha kupokea wajibu na majukumu yanayokuja na kusudi hilo.
Imani haiyafanyi mambo kuwa rahisi, bali inayafanya kuwa ya maana.
Na kwenye haya maisha, tunachohitaji siyo urahisi, bali tunachohitaji ni maana.

Unapokuwa unapitia magumu au changamoto, hata wengine wanapokuwa wanakosa imani na kukata tamaa, wewe ukijua kwa nini unapitia magumu hayo, kwa kujua maana yake kwako basi imani yako itakuwa imara na huwezi kutetereshwa na lolote.

Unapoimaliza siku hii ya leom tafakari ni kwa kiwango gani unajua maana ya maisha yako na kusudi la maisha hayo.
Kazana kujua maana na kusudi la maisha na hapo utaweza kujijengea imani imara isiyoshindwa na chochote.

Uwe na wakati mwema sana.
Kocha.