“People live by love: love of yourself is the beginning of death; love of other people and of God is the beginning of life.” – Leo Tolstoy
Ni jambo la kushukuru sana sisi kuweza kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Sisi binadamu tunaishi kwa upendo.
Kujipenda wewe mwenyewe ndiyo mwanzo wa kifo.
Kumpenda Mungu na kuwapenda wengine ndiyo mwanzo wa maisha.
Na kupenda kila unachofanya ndiyo mwanzo wa kuyafurahia maisha.
Upande haujakamilika kama ni wa upande mmoja tu, labda kujipenda mwenyewe au kuwapenda wengine tu.
Upendo lazima uwe wa pande zote ili uwe na manufaa kwako.
Upendo una nguvu kubwa sana, ambatana nao popote ulipo au unapokwenda.
Tukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujipenda sisi wenyewe, kuwapenda wengine na kupenda kile tunachofanya ili maisha yetu yawe bora sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania