“If you can teach a person kindness and love, but you do not, you lose a brother.” —CHINESE PROVERB
Kuiona siku hii mpya ya leo ni jambo la kushukuru sana.
Siyo kwa ngvu zetu wala akili zetu, bali ni bahati tu kwetu kuweza kuiona siku hii.
Tuitumie vyema kwa kufanya yale muhimu kwetu na kuachana na yasiyo muhimu.
Kama unaweza kufanya kitu, lakini ukaamua kutokukifanya umechagua kufanya makosa.
Kama unaweza kufundisha wema na upendo kwa wengine, lakini hufanyi hivyo unakosea na hivyo unapoteza nafasi ya kuzungukwa na watu wema na wenye upendo.
Chochote kile ambacho unaweza kukifanya na chenye manufaa kwa wengine, lakini unaamua kutokukifanya, iwe ni kwa uvivu au uzembe tu, ni makosa makubwa unafanya.
Siyo tu kinakuathiri wewe, bali pia kinawanyima wengine fursa ya kunufaika na kuwa bora zaidi.
Ni ubinafsi kutokufanya kile ambacho unaweza kufanya na kina manufaa kwa wengine.
Siku hii ya leo, nenda kafanye kile unachoweza kufanya na chenye kanufaa kwa wengine ili maisha yako na yao yaweze kuwa bora zaidi.
Leo ndiyo siku sahihi ya wewe kufanya na siyo kesho, hivyo usiahirishe yena kufanya leo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania