“Improve your own soul, and be confident that only in so doing can you contribute to the improvement of the larger society of which you are part.” – Leo Tolstoy

Watu wengi wamekuwa wanajiuliza wanawezaje kuibadili dunia, wanawezaje kuacha alama kwenye hii dunia.
Na jibu ni moja, ni kwa kuwa bora wewe mwenyewe ndipo wengine wanaweza kuwa bora pia.
Njia bora ya kupunguza umasikini pale ulipo ni kwa wewe kutokuwa masikini.
Njia bora ya kutengeneza upendo kwa wengine ni wewe kuanza kuwapenda wengine.
Na njia bora ya kuzungukwa na watu makini ni wewe kuwa mtu makini.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, kinatoa funzo kwa wengine ambao nao pia wanafanya.
Hivyo usijidharau na kuona huna mchango kwa kile unachofanya, dunia inakuangalia na wanaokuzunguka wanakuangalia, usiwaangushe.

Na hii ndiyo sababu nakusisitiza sana unapokuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, basi ujisukume kuwa bora, kwa sababu kwa wewe kuwa bora, utakuwa mfano mzuri kwa wengine kwamba inawezekana pia na wao kuwa bora.
Kwa wewe kufanya ambacho hakijawahi kufanywa inawapa wengine kujiamini kwamba na wao wanaweza.

Anza kuwa bora na wanaokuzunguka watakuwa bora pia.
Ukawe na wakati mwema, unapoimaliza siku hii, panga ni maeneo gani unakwenda kuwa bora zaidi kesho na kisha nenda kaianze siku yako kwa kile ulichopanga.

Kocha.