“The only real science is the knowledge of how a person should live his life. And this knowledge is open to everyone” – Leo Tolstoy

Sayansi ya kweli ni kuwa na maarifa ya jinsi ya kuyaishi maisha yako. Na maarida haya yako wazi kwa kila mtu.
Japo wengi wamekuwa hawapati nafasi ya kupata maarifa hayo na kujua jinsi ya kuyatumia.

Angalia jinsi ambavyo mimea na wanyama wanavyoishi kwa kanuni za asili.
Angalia jinsi ambavyo dunia inajiendesha kwa sheria za asili.
Na angalia namna ambavyo maisha ya kila kiumbe hai yanavyoanza mpaka yanavyoisha,
Na hapo utapata funzo kubwa sana kuhusu maisha.

Ukijua jinsi ya kuyaishi maisha yako, yatakuwa bora na utayafurahia.
Usipojua jinsi ya kuishi maisha yako, kila wakati utakuwa kama mtumwa.
Unapokwenda kuianza siku ya kesho, nia yako iwe moja, kupata maarifa sahihi ya jinsi ya kuyaishi maisha yako.

Uwe na wakati mwema.
Kocha.