“There is only one law, both in your personal and social life: if you want to improve your soul, you should be ready to sacrifice it.” – Leo Tolstoy

Asubuhi njema mwanamafanikio.
Ni siku nyingine nzuri sana kwetu, siku ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye maisha yetu.

Kama unataka kupiga hatua kwenye maisha yako, kama unataka maisha yako yawe bora zaidi, ni lazima uwe tayari kujitoa kafara.
Huwezi kuendelea kwa kujionea huruma,
Huwezi kupiga hatua kwa kufanya yale ambayo umezoea kufanya.
Ni lazima utoke nje ya mazoea,
Ni lazima ujisukume zaidi ya ulivyozoea,
Lazima ukubali maumivu ambayo hujawahi kuyapata.

Unafanya hivyo siyo kwa sababu hujipendi,
Bali ni kwa sababu unajipenda sana na hivyo unakuwa tayari kufanya lolote ili kufika kule unakotaka kufika.
Mafanikio yangekuwa rahisi kila mtu angekuwa nayo,
Kwa sababu kila mtu anatamani mafanikio,
Kila mtu anapanga kufanikiwa,
Lakini ni wachache sana wanaofanikiwa,
Kwa sababu wachache hao ndiyo walio tayari kujitoa kafara.
Swali ni je, wewe ni mmoja wa hao wachache?
Ni vitu gani upo tayari kujitoa kafara, uko tayari kuvikosa na maumivu gani upo tayari kuyavumilia ili ufanikiwe?
Tafakari hayo asubuhi ya leo na kisha chukua hatua sahihi ili kufika kule unakotaka kufika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania