“Associate with people who are likely to improve you.” — Seneca

Unapaswa kujihusisha na watu ambao wanakufanya kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa.
Watu ambao wabakuonesha kipi sahihi cha kufanya,
Wanaokuambia ni vitabu gani vizuri ufanye,
Wanaokupa mawazo mazuri ya kupiga hatua,
Na wasioogopa kukuambia pale unapokosea.

Unapaswa kuwaepuka watu ambao wanakufanya uwe hovyo kuliko ulivyo sasa.
Watu ambao wanapinga, kukosoa na kukatisha tamaa kila mpango unaowaeleza.
Watu ambao kila wakikutafuta ni kwa ajili ya kula ‘bata’ tu,
Watu ambao ukikosea hawakuambii, ila wanaenda kuwaambia wengine.

Uzuri ni kwamba una uhuru wa kuchagua watu gani ujihusishe nao.
Na pia unawajua wapi wanakufanya uwe bora na wapi wanakufanya uwe hovyo.
Fanya uchaguzi sahihi sasa ili uweze kupiga hatua.

Uwe na usiku mwema na unapolala jipe jukumu la kupunguza wale wanaokurudisha nyuma.
Kocha.