“It is not the place we occupy which is important, but the direction in which we move.” —OLIVER WENDELL HOLMES
Tumeipata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu,
Tunapaswa kwenda kuitumia siku hii vyema ili kuweza kufanya makubwa na kupata matokeo bora sana.
Kilicho muhimu kwako siyo pale ulipo sasa, bali kule unakokwenda,
Haijalishi sana uko wapi sasa, bali ni uelekeo upo unaokwenda.
Uelekeo wako ni muhimu kuliko pale ulipo sasa.
Hata kama huna fedha na kipato chako ni kidogo na upo kwenye umasikini, kama kwenye kila kipato chako kuna sehemu kidogo unayoiweka pembeni kama akiba basi upo kwenye uelekeo mzuri.
Ni swala la muda tu, utakuwa sehemu tofauti na ulipo sasa.
Haijalishi kwamba hujui mambo mengi kiasi gani na unajiona mjinga sana, kama kila siku unatenga muda na kujifunza, utazidi kupata maarifa yanayokuwezesha kuwa bora zaidi.
Baada ya muda utakuwa umendoka kwenye ujinga na kuwa na hekima kubwa.
Hata kama upo nyuma kiasi gani kwenye kazi au biashara yako, kama kila siku unakazana kuwa bora zaidi ya jana, ni swala la muda tu, utakuwa umepiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Hivyo rafiki, usiumizwe sana na pale ulipo sasa, bali angalia ni wapi unapokwenda, na siyo kwa mipango, bali kwa hatua unazochukua.
Kama hatua unazochukua ni sahihi, hata kama ni ndogo kiasi gani, hizo ndiyo muhimu, zitakazokutoa hapo ulipo sasa.
Ukiendelea na hatua hizo, huwezi kubaki hapo ulipo sasa.
Hivyo wajibu wako kila siku ni kukagua uelekeo wako kama rubani au nahodha anavyokagua uelekeo wa chombo chake kila wakati.
Kwa sababu uelekeo usipokuwa sawa, hata matokeo ya mwisho hayawezi kuwa sawa.
Ni wapi upo sasa na uelekeo wako unakupeleka wapi? Tafakari hili asubuhi ya leo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania