A wise man seeks wisdom; a madman thinks that he has found it. —PERSIAN PROVERB
Werevu hutafuta hekima mara zote,
Lakini wapumbavu huamini tayari wanajua kila kitu.
Kuna vitu vingi sana vya kujua, hivyo mwerevu anajua hawezi kujua vyote.
Hilo linamfanya awe mnyenyekevu na tayari kujifunza wakati wote na kutoka kwa yeyote au chochote.
Mpumbavu akishajifunza kiasi fulani na akapata matokeo fulani mazuri, anaanza kujiona tayari ameshajua kila kitu.
Hivyo hajifunzi tena, anakuwa na kiburi na kujiamini kupitiliza,
Haya yote yanamuandaa kwa anguko kubwa baadaye.
Usiwe mpumbavu, kuwa mwerevu na jua kuna mengi hujui hivyo kuwa tayari kujifunza.
Pia jua kila unayekutana naye na kila hali unayopitia, kuna kitu cha kujifunza, kitafute na ujifunze.
Ukawe na usiku mwema, usiku wa kujiandaa kwa kujifunza zaidi kesho.
Kocha.