“We live a short period of time in this world, but we live it according to the laws of eternal life.” —After HENRY DAVID THOREAU

Siku hii nyingine mpya kwetu ni zawadi ya kipekee sana kwetu.
Tunayo nafasi ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana,
Ukilinganisha na muda ambao dunia imekuwepo ambao ni mabilioni ya miaka, hata ukiishi miaka 100 bado ni kama nukta tu kwenye mstari mrefu wa dunia hii.

Njia pekee ya kuacha alama hapa duniani, ambayo itakumbukwa hata baada ya wewe kuwa umeshaondoka hapa duniani, ni kugusa maisha ya wengine kwa namna ambayo unaacha alama kwenye maisha hayo.
Kama unataka kuishi milele,
Kama unataka jina lako liendelee kuwepo hata baada ua wewe kuondoka, basi ishi kwa kanuni za asili na ishi maisha yako kwa namna ambayo yana manufaa kwa wengine.

Huo unapaswa kuwa utaratibu wa maisha yako, unafanya kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya na siyo kwa sababu unataka ukumbukwe.
Upo usemi kwamba maisha ni kile kinachotokea wakati sisi tupo bize na mipango mbalimbali.
Kadhalika, utajikuta unaishi milele kama hujapanga kufanya hivyo, bali umepanga kuishi maisha yako na kufanya kilicho sahihi.

Uwe na siku bora sana leo, siku ya kufanya kilicho sahihi ambacho kinayafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Www.t.me/somavitabutanzania