Kutokusamehe ni sawa na kunywa sumu ya panya, huku ukisubiria maadui zako wafe.
Watu wengi wanaishi kwa chuki na vinyongo vinavyowapelekea kufa kiakili, kiroho na kimwili kwa sababu ya kutokusamehe.

Hakuna kazi ngumu kama ya kuwabeba watu, wewe unaishi ukiumia wakati wenzako wakifurahia kula maisha yao.
Na tunapoambiwa samehe siyo ni kwa faida ya mtu mwingine, Bali ni kwa faida yako.
Samehe kwa faida yako wewe mwenyewe ili mambo yako yaende, ukisema uwabebe watu wote utakosa hata mtu wa kuongea naye, kila mtu utamuona ni mbaya.

Kitu ambacho ni cha uhakika kama leo hii unavyoenda kuanza siku yako ni watu wa kukuudhi, hakuna siku itakayokwenda hewani bila ya watu kukukosea au kuwakosea.

Na hapa ndipo panapokuja umuhimu wa msamaha, ili urudishe uhusiano uliopotea, urudishe uhusiano wa awali inakupasa usamehe na msamaha utakao tumia hapa ni msamaha wa kweli.

Sehemu pekee ambayo msamaha wa kweli unatoka ni moyoni.
Unaweza kusema nimesamehe kwa nje lakini kama ndani hujasamehe kweli ule uchungu utaendelea kukutafuna.

Msamaha wa kweli unatoka ndani, tunapoamua ndani kusamehe basi ule msamha unakuwa wa kweli.

Ni wakati wa kuondoa uchungu uliombika ndani ya moyo kupitia msamaha wa kweli. Msamaha wa kweli unatoka moyoni na unaponya majeraha ya na nafsi.

Anayesamehe bila kutoka moyoni ndiyo anaendelea kuumia zaidi kuliko yule anayesamehe bila kutoka ndani ya moyo.

Usiishi maisha ya wivu, chuki na vinyongo, amua leo kuwa huru kwa kuwasamehe wale walikuumiza na kukuudhi. Usiendelee kubaki na sumu ya panya ambayo itakuja kukuua wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; Jua kiini cha kosa halafu nenda kasamehe.
Kwani kuna muda mwingine mtu huwa anakuwa na chuki tu na mtu mwingine na ukichunguza kiini cha kosa unakuja kugundua ni wivu.

Kwahiyo, unapaswa kufanya maamuzi ya makusudi kabisa ya kuamua kusamehe, wasamehe wale waliokufanyia ubaya na endelea na maisha yako.

Unapokataa kutokusamehe maana yake umechagua adui yako kuendelea kukutawala ndani ya akili yako. Badala ya kuwaza kazi muhimu utakua unatumia muda mwingi kumfikiria adui yako na
hii inakuwa hasara kiuzalishaji.

Kila la heri rafiki yangu.

Makala hii imeandikwa na,
Mwl. Deogratius Kessy ambaye ni mwalimu, mwandishi na mjasiriamali. Unaweza kuendelea kujifunza kwake kupitia tovuti yake http://kessydeo.home.blog na vitabu alivyoandika.

Unaweza kuwasiliana naye kwa 0717101505 na 0767101504
Au barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Karibu sana na Asante sana rafiki yangu.