“Submission to the law created by men makes one a slave; obedience to the law created by God makes one free.” – Leo Tolstoy
Ukifuata sheria zilizowekwa na wanadamu, unakuwa mtumwa wa hao walioweka sheria hizo.
Ukitii sheria zilizowekwa na Mungu (sheria za asili) unakuwa na maisha huru.
Watu wengi hawapo huru kwa sababu wanatii kila sheria ya wanadamu huku wakivunja kila sheria ya asili,
Hivyo wanachagua kuwa watumwa kwa binadamu wengine huku pia wakipata adhabu kwa kuzivunja sheria za asili.
Unapokwenda kuimaliza siku ya leo, tafakari ni kwa namna gani umekuwa unajinyima uhuru kwa kufuata sheria za wanadamu huku ukizivunja sheria za asili.
Rudisha uhuru wako kwa kuzijua na kuzifuata sheria za asili,
Na uzuri ni kwamba ukizifuata sheria za asili sheria za wanadamu hazitakupa tabu.
Uwe na usiku mwema.
Kocha.