“You’ll stop caring what people think about you when you realize how seldom they do.” – David Foster Wallace
Umekuwa unaogopa kuyaishi maisha yenye maana kwako, kusimamia misingi ambayo ni sahihi kwako na hata kufanya mambo kwa utofauti.
Kinachokuogopesha ni jinsi gani wengine watakuchukulia na kukufikiria.
Unaona ni bora uendelee kuwa kama wao, ili wakuchukulie wewe ni kawaida.
Lakini leo nakupa siri moja itakayovunja hofu hiyo.
Siri yenyewe ni hii, WATU HAWAJALI KIIVYO,
Kabisa, siyo kama unavyofikiria.
Wanaweza kukusema vibaya, kukukosoa au kukukatisha tamaa.
Lakini nikuhakikishie hakuna anayekosa usingizi kwa sababu anafikiria sana mambo yako.
Kila mtu anapambana na hali yake na hivyo chagua kuyaishi maisha yako halisi bila ya kuhofia wengine wanakuchukuliaje.
Uwe na usiku mwema.
Kocha.