Seneca said, “Hold fast, then, to this sound and wholesome rule of life…The body should be treated more rigorously, that it may not be disobedient to the mind.”
Tabia ya kuuonea mwili wako huruma, ndiyo inaufanya uwe na ukaidi kwa akili na roho.
Unajua kabisa nini unataka, umeshapanga namna ya kupata, lakini wakati wa kufanyia kazi mipango, mwili unakuambia umechoka, na wewe unakubaliana nao kirahisi.
Huwezi kufanikiwa kwa kuuonea huruma mwili wako,
Ukisema unaamka saa kumu alfajiri, ikifika amka, usianze kujadiliana ma mwili kama unataka kuamka au la. Akili na roho yako vimeridhia uamke saa kumi alfajiri, amka saa kumi alfajiri.
Umeshajiambia kuna jukumu unataka ulikamilishe kabla siku haijaisha, halafu unaiona siku inayoyoma na kujiambia utafanya kesho! Kwani kuna mwingine alikupangia? Si ulipanga mwenyewe, basi usiusikilize mwili, fanya.
Ukiuendekeza sana mwili, unakufanya kuwa mtumwa na ukishakuwa mtumwa wa mwili, habari yako imekwisha.
Ukawe na usiku mwema, kama kuna kitu ulipanga kufanya leo, halafu umekiahirisha kwa kuusikiliza mwili, usilale kabla hujakifanya, upe adhabu mwili wako leo ili usirudie tena kuwa kikwazo kwako.
Na muda uliojiambia utaamka kesho, ukifika amka, usiusikilize mwili.
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania