“There are two different states of human existence: first, to live without thinking of death; second, to live with the thought that you approach death with every hour of your life.” Leo Tolstoy

Ni bahati iliyoje kwako kuweza kuiona siku hii mpya ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwako kwenda kuweka juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo bora sana.
Usiipoteze siku hii ya leo, kwa sababu huenda usiipate siku nyingine kama hii.

Kuna njia mbili za kuyaishi maisha yako.
Njia ya kwanza ni kwa kutokufikiria kifo kabisa, na hivyo kuishi kama vile hakuna kufa, kuahirisha mambo na kuona bado una muda wa kutosha kufanya chochote unachotaka.
Njia hii haikusukumi na hivyo utapoteza muda wako kwa mambo yasiyo muhimu.

Njia ya pili ni kujua kwamba kila saa unakikaribia kifo chako. Kwa njia hii unajua kabisa kwamba huna muda na hivyo kuutumia vizuri muda mdogo ulionao.
Kwa kuwa huna uhakika wa kuwepo kesho, unafanya yale muhimu leo bila ya kuahirisha. Kwa kujua muda wowote unaweza kuondoka, hutaupoteza kwa yasiyo muhimu, badala yake utaweka vipaumbele vyako vizuri.
Njia hii inakupa msukumo mkubwa wa kuyaishi maisha yako leo na siyo kuyaahirisha kwa siku zijazo, maana huna uhakika nazo.

Ishi kwa njia hiyo ya pili, kwa sababu hujui ni muda kiasi gani uliobakiza,
Ishi leo kama ndiyo siku yako ya mwisho, ukifanya yale muhimu ambayo hitaki kuyaacha hayajafanywa.
Na kama kesho utapata siku nyingine basi ni bahati kwako na unakwenda kuitumia vizuri pia.

Mafanikio kwenye maisha siyo kitu kinachotokea mara moja kaka ajali, bali ni kitu kinachojengwa na siku moja moja unazoziishi kwenye mafanikio.
Je siku hii ya leo itahesabika kwenye mafanikio yako?

Uwe na siku bora ya leo, siku ya kuishi kikamilifu ukijua unaweza usiione siku nyingine kama hii.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania