“We are not free in this world, subdued by our passions and by the emotions of other people to the degree that we forget the requirements of our intellects. If we really want to become free, we can be so only through our intellect.” – Leo Tolstoy
Ni nafasi nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tunapaswa kuitumia siku hii vyema ili tuweze kufanya makubwa na kupata matokeo bora sana.
Kama unataka kuwa huru, basi tumia akili yako.
Utegemezi wako kwenye hisia, zako mwenyewe na hata za wengine ndiyo unaokunyima uhuru wako.
Tamaa, hofu, hasira na hisia nyingine, ndiyo gereza ambalo umejijengea wewe mwenyewe.
Unapozipa hisia hizi nafasi kubwa, unajikuta ukifanya mambo ambayo baadaye unajuta kwa nini ulifanya.
Uhuru wako upo kwenye akili yako,
Pale unapofikiri jambo kwa kina, unaona wazi kilicho sahihi kufanya kulingana na hali halisi.
Unapofikiri, unapata nafasi ya kuelewa kitu kwa kina na hivyo kuweza kufanya maamuzi sahihi.
Unapotumia hisia, unasukumwa kufanya maamuzi ambayo siyo sahihi.
Uwe na siku bora ha leo, siku ya kutumia akili yako ili uwe huru na kutoruhusu hisia zikutawale na ukawa mtumwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania