Rafiki yangu mpendwa,

Kuna kitu kimoja nakijua kwa uhakika na bila ya shaka yoyote kuhusu wewe. Kitu hicho ni kwamba, una ukuu ndani yako, una uwezo mkubwa sana ambao umelala ndani yako, ambao bado hujaanza kuutumia ipasavyo.

Utajiuliza nimejuaje hili na ninapata wapi uhakika, na jibu ni hili, nimeona kwa walio wengi ambao nimefanya nao kazi kwenye eneo la ukocha. Nimeona jinsi ambavyo watu wanapokuwa na msukumo wa nje wanajituma zaidi na kufanya makubwa zaidi kuliko wakiwa peke yao.

9D1A5847

Mwezi Januari 2020 tuliendesha programu ya ukocha inayoitwa GAME CHANGERS, hii ni programu ambayo inakupa manufaa mawili kwa wakati mmoja, unapata ukocha pamoja na kundi la wengine wanaofanya makubwa kama wewe.

Kutoka kwa washiriki wa programu hii wa mwezi januari 2020 nimezidi kuona jinsi ambavyo kila mtu ana uwezo mkubwa ndani yake ambao hajaanza kuutumia.

Programu ilikuwa na washiriki wanne, na kwa kifupi haya ni matokeo makubwa ambayo kila mshiriki aliweza kupata kwa wiki nne za programu hii.

Washiriki wawili wameweza kuandika vitabu na kuvikamilisha ndani ya wiki hizo nne.

Mshiriki mmoja ameweza kuanzisha duka la rejareja ndani ya wiki hizo nne.

Mshiriki mmoja ameweza kuweka mfumo  bora kwenye ufugaji wake wa kuku na kuondoa vifo kabisa kwa vifaranga.

Mshiriki mwingine ameweza kuwashirikisha wengine biashara ya mtandao anayofanya na kuweza kupata mtu wa kujiunga na wengine wa kununua bidhaa, kitu ambacho kilikuwa kigumu kwako huko nyuma.

Rafiki, unapoona matokeo ya aina hii, ndani ya muda mfupi kwa watu ambao hawajawahi kufanya hivyo kwenye maisha yako, ndipo unapata uhakika kwamba kila mtu ana ukuu ndani yake, anachokosa ni msukumo sahihi wa kutumia ukuu huo.

Rafiki, sasa ni nafasi yako na wewe kutumia ukuu ambao upo ndani yako.

Ni nafasi yako kutoruhusu mwaka huu 2020 uishe hivi hivi kama miaka mingine, ni nafasi yako ya kuufanya mwaka huu kuwa bora na wa kipekee kwako, mwaka wa kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Napenda kukujulisha kwamba tutakuwa na msimu mwingine wa programu ya GAME CHANGERS ambayo itafanyika mwezi Machi 2020.

Usajili wa kupata nafasi ya kushiriki programu hii kwa mwezi machi umeshaanza rasmi, hivyo wewe kama rafiki yangu na mtu ambaye umejitoa kufanya makubwa, hupaswi kukosa nafasi hii.

Nafasi za kushiriki programu hii ni TANO (05) pekee kwa wakati mmoja, hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii nzuri na ya kipekee sana kwako, chukua hatua sasa.

Nitaendelea kukupa maelezo zaidi kuhusu programu hii, utaratibu wake na jinsi utakavyonufaika nayo. Nitakupa shuhuda za wale walioshiriki na jinsi ilivyowanufaisha.

Kwa sasa nataka uchukue hatua moja, kama kweli unataka kufanya makubwa mwaka huu 2020 na upo tayari kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS Machi 2020 basi tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap namba 0717396253, ujumbe useme NATAKA KUFANYA MAKUBWA 2020.

Rafiki, usiache nafasi hii ipite, usikubali mwaka 2020 uwe kama miaka mingi uliyoipoteza huko nyuma, unayo nafasi ya kufanya makubwa, karibu sana tufanye kazi pamoja. Kanuni ninayo, na ushahidi wa walionufaika ninao, kazi ni kwako kuchukua hatua. Tuma ujumbe sasa, kwa wasap kwenda namba 0717 396 253 ujumbe uwe na maneno NATAKA KUFANYA MAKUBWA 2020, kisha nitakupa maelezo zaidi pamoja na nafasi ya kushiriki.

Kama nilivyokuambia, nafasi ni 5 pekee, hivyo zikishajaa, hakuna tena nafasi nyingine. Chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii ya kipekee kwako. Njoo tufanye kazi pamoja ili mwaka 2020 uwe mwaka bora sana kwako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania