“Pure perfection can be found only in God; one’s life consists of becoming closer to God. And when a person knows that good is good and that evil is evil, then he or she gets closer to good, and moves farther from evil.” —CONFUCIUS
Tumepata nafasi nyingine mpya ya kuiona siku hii mpya ya leo.
Ni fursa ua kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Hakuna aliyekamilika ila Mungu pekee.
Sisi wengine tuna wajibu wa kukazana kuwa bora zaidi kila siku.
Muhimu ni kujua wema na uovu, kisha kukazana kuwa mwema na kuondokana na uovu.
Kitu kibaya kabisa kwenye maisha ni kutenda maovu bila ya kujua kwamba unatenda maovu.
Hapo utaendelea kurudia maovu hayo na kuharibu kabisa maisha yako.
Lakini unapojua maovu na kutambua pale unapoyafanya na kisha kujirekebisha, unakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kuwa bora zaidi.
Kukosea kupo, hata baada ya kujua mema na maovu bado kuna wakati utateleza na kufanya maovu.
Muhimu ni kujua wakati umefanya hivyo na kujirekebisha wewe mwenyewe.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kutambua maovu na kuepuka kuyarudia ili uwe bora zaidi leo kuliko jana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania