Habari za leo rafiki yangu mpendwa?

Ninayo furaha kubwa sana leo kukuletea taarifa muhimu sana kwa mafanikio yako.

Taarifa hiyo ni kuhusu programu maalumu ya ukocha ambayo huwa inakuja kwa misimu maalumu inayokwenda kwa jina la GAME CHENGERS.

game changers.jpg

TATIZO.

Kuna kitu kimoja ambacho nimekuwa nakiona kwa watu wengi wanaojiunga na huduma mbalimbali za mafunzo, ushauri na ukocha ninazotoa.

Awali wanakuwa na hamasa kubwa ya kujifunza na kuchukua hatua na hilo linawaletea matokeo makubwa sana kuliko walivyozoea huko nyuma.

Hali hiyo ya matokeo makubwa inawafanya wapate hamasa zaidi na kuchukua hatua zaidi kitu kinacholeta matokeo zaidi.

Lakini baada ya ukuaji wa haraka wa awali, wanafikia ukomo. Wanafika hatua ambayo hawakui zaidi. Wanakazana kuweka juhudi sana lakini hawakui zaidi ya pale. Na hapo hamasa inaanza kushuka na wengi kujikuta wanarudi nyuma.

Wengi wanapofika kwenye hatua hii, hukata tamaa na kuacha kabisa kufuatilia au kupata huduma ninazotoa, maana wanakuwa wamejishawishi hakuna tena namna ya kuvuka pale walipofika.

IPO NJIA.

Kitu ambacho nataka kukuambia rafiki yangu, kama umeshafika kwenye ukomo huu ni kwamba ipo njia.

Ipo njia ambayo siyo rahisi, lakini ni ya uhakika, na njia hiyo ni kubadili kabisa mfumo wako wa fikra, mfumo wako wa maisha na mtazamo ulionao kuhusu wewe na kile unachofanya. Kwa Kiingereza tunasema unahitaji MENTAL SHIFT.

Kinachokukwamisha wewe ni ukomo wa kifikra na kimtazamo ambao umeshaufikia, bila ya kubadili hiki, hakuna juhudi zitakazoweza kukutoa hapo ulipo.

Njia pekee ya kuondoka kwenye mkwamo uliofikia ni kubadili kabisa mfumo wako wote wa maisha, kitu ambacho unahitaji usimamizi wa karibu wa kukifanya, kwa sababu ukikifanya mwenyewe utajionea huruma na kuishia njiani.

SULUHISHO.

Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye suluhisho la mkwamo ambao umefikia.

Suluhisho hilo ni programu maalumu ya ukocha ambayo inaitwa GAME CHANGERS.

Kupitia GAME CHANGERS unapata nafasi ya kubadili kabisa mfumo wa maisha yako na kuweza kukua zaidi ya pale ulipokwama sasa.

GAME CHANGERS inakupa vitu viwili kwa wakati mmoja, COACHING NA MASTER MIND.

COACHING unakuwa na kocha anayekuongoza kwenye mabadiliko unayokwenda kupitia, anayekupa mwongozo sahihi na kukusukuma zaidi.

MASTER MIND unakuwa ndani ya kundi la watu wanaotaka kubadilika kama wewe, ambao wanakupa hamasa na msukumo wa kuchukua hatua zaidi.

Katika programu hii ya GAME CHANGERS utakuwa na mimi kocha wako Dr. Makirita Amani katika kipengele cha COACHING, na pia utakuwa na watu wengine wanne ambao wanataka kubadilika kama wewe katika kipengele cha MASTER MIND.

Kwa siku 30, utapata msukumo wa kubadili kabisa maisha yako na baada ya hapo utaweza kwenda kwa kasi kubwa na kupata ukuaji zaidi kwenye lile eneo ambalo umekwama.

WATU AMBAO GAME CHANGERS INAWAFAA.

GAME CHANGERS siyo programu inayomfaa kila mtu. Bali ni programu maalumu kwa wale ambao wameshapiga hatua kiasi fulani na kufikia mkwamo na wangependa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao kwa kujitoa zaidi.

Watu waliokwama kwenye maeneo yafuatayo programu hii inawafaa zaidi;

  1. Upo kwenye biashara ambayo imefika ukomo na haikui zaidi.
  2. Upo kwenye kazi ambayo huoni ukikua, umefikia hatua unaifanya tu kwa mazoea.
  3. Upo kwenye mahusiano ambayo unaona hayaendi mbele, iwe ni mahusiano ya mapenzi au ndoa.
  4. Umekwama kiafya na huoni ukiweza kupiga hatua zaidi, labda umekuwa ukijaribu kupunguza uzito lakini haupungui.
  5. Kuna tabia unataka kujijengea lakini kila ukianza unaishia njiani.
  6. Kuna kitabu unataka kuandika lakini hujaanza au umeanza na kuishia njiani.
  7. Kuna biashara mpya umekuwa unapanga kuanza lakini kila siku hufikii maamuzi ya kuanza.
  8. Kuna kozi mpya unataka kujifunza lakini kila wakati unaona huna muda au hujawa tayari.
  9. Malengo uliyojiwekea kwa mwaka hujaweza kuyafanyia kazi kwa uhakika.
  10. Upo kwenye mkwamo mkubwa kimaisha, licha ya kupiga hatua zaidi lakini unaona changamoto ni nyingi na matatizo hayaishi, huna furaha kabisa.

Kwa siku 30 utachagua eneo moja la kufanyia kazi, eneo ulilokwama na unahitaji kujikwamua ili upige hatua zaidi kwenye maisha yako. Na kwa siku hizo 30 utaweza kupiga hatua kubwa sana kuliko unavyoweza kupiga kwa mwaka mzima ukiwa mwenyewe.

UTARATIBU WA GAME CHANGERS.

Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne katika kutoka pale ulipokwama.

Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.

Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao.

Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.

Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.

Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.

Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.

NAFASI ZA KUSHIRIKI GAME CHANGERS MACHI 2020.

Rafiki, kama nilivyokushirikisha kwenye utangulizi, programu hii ya GAME CHANGERS huwa inaendeshwa kwa misimu, na msimu mmoja unachukua siku 30 ambazo ni mwezi mmoja.

Tunakwenda kuanza msimu mwingine wa programu hii ya GAME CHANGERS mwezi Machi 2020, kuna nafasi tano pekee za kushiriki programu hii kwa msimu huo wa mwezi machi. Hivyo karibu sana uchukue hatua sasa.

HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUSHIRIKI GAME CHANGERS.

Kama kwa kusoma hapa umeona GAME CHANGERS ni kitu unachohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa (na ni kitu unachohitaji kweli), basi chukua hatua sasa ili kuweka nafasi yako ya kushiriki programu hii.

Hatua ya kuchukua ni kutuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako na maelezo kwamba utashiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020.

Kwa kufanya hivi unajihakikishia nafasi ya kushiriki programu hii na kunufaika nayo.

Chukua hatua sasa kwa sababu nafasi zilizopo ni chache (tano pekee) na uhitaji ni mkubwa. Tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA MSIMU WA MACHI 2020.

Ada ya kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.

Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.

Msimu wa mwezi Machi wa programu hii ya GAME CHANGERS 2020 utaanza rasmi siku ya jumamosi tarehe 07/03/2020 na kumalizika siku ya jumamosi ya tarehe 04/04/2020.

Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/= kabla ya tarehe 03/03/2020. Pia tuma mapema taarifa ya ushiriki ili uweze kupata nafasi hii, kwa kutuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba utashiriki GAME CHANGERS JANUARI 2020.

Nafasi za kushiriki programu hii kwa mwezi machi ni 5 pekee, na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.

Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache chache sana.

Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020 ni tarehe 03/03/2020. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 05/03/2020 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.

Tarehe 07/03/2020 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.

Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.

Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.

Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha

game changers.jpg