“Why do people like to blame others so much? He who casts blame on another person is quick to think that he would not do the very same thing. It is the same with people who like to listen to the fault-finding of their neighbors.” – Leo Tolstoy

Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Unapenda kulaumu wengine kwa sababu unafikiri wewe huwezi kufanya kama walivyofanya wao.
Lakini huo siyo ukweli,
Mara nyingi kile ambacho unalaumu kwa wengine, ndiyo hicho hicho ambacho na wewe unafanya pia.
Unatumia kuwalaumu wengine kama njia ya kuhalalisha wewe kufanya kile ambacho wengine wanafanya na unawalaumu.

Tambua kwamba lawama zozote unazotoa kwa wengine hazina manufaa yoyote kwako.
Haziwabadilishi na wala hazikupi wewe kile unachotaka.
Pokea kila kinachotokea kwenye maisha yako kama wajibu wako na chukua hatua sahihi kubadili chochote kilichotokea.
Na kabla hujalaumu wengine, hebu anza kuyaangalia maisha yako mwenyewe, je hakuna maeneo ambayo unafanya kile unachotaka kuwalaumu wengine kwa kufanya?
Mara nyingi utajikuta na wewe ni mfanyaji wa kile unacholaumu.
Hivyo kulaumu kunakuwa hakuna maana yoyote kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuacha kuwalaumu wengine kwa lolote lile na kubeba jukumu la maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania