Kila mmoja wetu ni kiongozi, na kiongozi anaanzia ndani ya mtu mwenyewe pili ngapi ya familia nakadhalika.

Kuna kitu ambacho viongozi wengi sasa ndiyo wameona ndiyo habari ya mjini, wanafikiri wataleta ufanisi kwa njia hiyo kumbe ni kuwapoteza wale wanaowaongoza.

Uongozi ambao hauleti ufanisi ni ule ambao kiongozi anakuwa anajenga hofu ndani ya wale anaowaongoza. Uongozi wa kuwajengea hofu wale unaowangoza hauleti ubunifu wa aina yoyote.

Kwani mtu mwenye hofu huwa hawezi kusema ukweli, na mtu akishindwa kusema ukweli hawezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Usiwe kiongozi wa kuwaelekeza wale unaowangoza kwa kuwajengea hofu, ukishawajengea hofu watu wanashindwa kutoa uwezo wao wa ndani, wanashindwa kwenda hatua ya ziada. Waongoze kwa upendo, wape uhuru wa kutumia akili zao vizuri na siyo kuwaamulia kila kitu.

Hata katika familia usiwe baba au mama wa kuongoza familia yako kwa kujaza hofu kwa wale unaowangoza. Kuna familia nyingine, watoto wakishamuona baba wote wananywea hata furaha zao zinayeyuka kama vile mshumaa kwenye upepo. Watoto wanapoteza uwezo wa kujiamini pale mzazi anapokuwa mkali kupita kiasi.

Kisaikolojia iko hivi, kila binadamu anahitaji kuthaminiwa. Ukishamuona yule uliyenaye kwamba una mthamini ataweza kukufanyia mambo makubwa sana.
Kumbe basi, hitaji la kila binadamu ni kuhisi anathaminiwa.

Falsafa nzuri ya Uongozi ni kuongoza kwa upendo, kubali kutumika kwa ajili ya wengine, na uongozi ni kutumika na siyo kusubiri kutumikiwa. Unaposubiri kutumikiwa ni mzigo ambao kila mtu atashindwa kuubeba.

Hatua ya kuchukua leo;usitumie mabavu kwa wale unaowaongoza kwenye ngazi yoyote ile, usiwajengee hofu wale unaowangoza, wajengee uwezo wa kujiamini na kutumia vipaji vyao vizuri.
Kila mtu ana anajua ni kuamsha tu ule uwezo mkubwa ulioko ndani yake.

Kwahiyo, hatuwezi kuwa na jamii bora kama tutaongoza kuanzia ngapi ya familia kwa kuwajengea watu hofu.
Usiwajengee watu hofu, wape amani, matumaini na uhuru wa kufanya kazi na maamuzi.

Ukawe na siku bora sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com
kessydeoblog@gmail.com
kessy@ustoa.or.tz
http://kessydeo.home.blog
Karibu sana na
Asante sana.