“The fulfillment of our duties and the satisfaction of our personal pleasures are two different things. Duties have their own laws, and even if we try to mix our duties with our pleasures, they will separate themselves.” —After IMMANUEL KANT
Ni siku nyingine mpya ambapo tumepata nafasi ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Yale unayofanya kwenye maisha yako yamegawanyika kwenye makundi mawili,
Kundi la kwanza ni kutekeleza wajibu wako,
Kundi la pili ni kutafuta raha.
Makundi haya mawili huwa hayachangamani,
Wajibu una kanuni na sheria zake, unachofanya ili kutimiza wajibu lazima kifuate kanuni na sheria hizo.
Lakini raha hazina kanuni wala sheria, unachofanya ili kupata raha hakihitaji nguvu kubwa.
Unapojaribu kuchanganya wajibu na raha, au unaposhindwa kutofautisha vitu hivyo viwili, ndiyo chanzo cha wewe kushindwa kupiga hatua.
Ni muhimu sana kabla hujafanya kitu chochote ujiulize je unatimiza wajibu au unajipa raha.
Unapoingia kwenye mitandao ya kijamii wakati una kazi za kufanya jiulize unatekeleza wajibu au unajipa raha?
Mafanikio yako ni matokeo ya kuweka muda na nguvu zako kwenye kutekeleza wajibu wako kuliko unavyoweka kwenye kujipa raha.
Maana raha ni za muda mfupi lakini unapotekeleza wajibu, matokeo yake ni ya muda mrefu.
Uwe na siku bora sana leo, siku ya kutekeleza wajibu wako na kuacha kukimbizana na raha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania