“It is obvious for everyone that death expects us all in the long run; but nevertheless we live our lives as if there will be no death.” – Leo Tolstoy
Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwako kwenda kuweka juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo bora sana.
Itendee haki siku hii kwa kufanya yale ambayo ni muhimu kwako kufanya.
Umekuwa unaishi kama vile hakuna kifo,
Unaahirisha mambo muhimu na kujiambia utafanya kesho, kama vile una uhakika wa kuiona hiyo kesho.
Unajisumbua na mambo yasiyo muhimu kama vile una muda usio na ukomo.
Unapotambua kwamba huna uhakika na kesho, unajisukuma kufanya yale muhimu leo.
Unapotambua kwamba muda wako una ukomo, unaacha kuupoteza kwa yale yasiyo muhimu.
Ni wakati wa kuacha kujidanganya na kuukabili uhalisia, kwamba muda uns ukomo na kesho huna uhakika nayo.
Hivyo kila unapoiona inayoitwa leo, kwanza unashukuru kwa kuiona na pili unaitumia vizuri kwa sababu ndiyo siku pekee ambayo una uhakika nayo.
Kwa chochote unachofanya, kabla hujaendelea kufanya, jiulize kama ungejua leo ndiyo siku yako ya mwisho, ungetumia muda huo kufanya kitu hicho.
Mfano unabishana na watu ili uonekane uko sahihi, kwa jambo lisilo na umuhimu, kama utakufa kesho, kuwa sahihi leo inakisaidia nini? Si yapo mengine muhimu zaidi ungeweza kuyafanya, kama kuwasiliana na wale muhimu kwako, kukamilisha kitu muhimu ulichokuwa umeanza n.k.
Unapofikiria kuhusu kifo, ambacho ni njia ya kila mtu, unayafikiria tofauti kuhusu maisha yako na kila unachofanya.
Uwe na siku bora ya leo, siku ya kufanya yale muhimu ambayo ungeyafanya kama leo ingekuwa ndiyo siku yako ya mwisho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania