“Man needs difficulties, they are necessary for health.” – Carl Jung
Kuiona siku hii nyingine mpya ya leo ni jambo la kipekee na kushukuru sana.
Nenda kaitumie vyema siku hii, uweze kufanya makubwa na kupata matokeo bora sana.
Hakuna mtu anayependa kupitia magumu au changamoto kwenye maisha yake.
Lakini ni magumu hayo ndiyo yanakufanya kuwa imara zaidi.
Hata ukiangalia kwenye asili, mti ulioota eneo lisilo na maji unakuwa imara kuliko ulioote eneo lenye maji mengi.
Mti ulioota eneo lenye upepo mkali ni imara kuliko ulioota eneo lisilo na upepo.
Na mtu ambaye hajawahi kupata maradhi yoyote, mwili wake unakuwa dhaifu kuliko yule ambaye alishapata maradhi na mwili ukatengeneza kinga.
Mtu ambaye amewahi kupata hasara kwenye biashara anakuwa makini kuliko ambaye hajawahi kupata hasara.
Kila ugumu unaokutana nao, unakuacha ukiwa imara zaidi kuliko ulivyokuwa kabla ya ugumu huo.
Hivyo usilalamike pale unapokutana na magumu, bali jua ni fursa kwako kuwa bora na imara zaidi.
Uwe na siku bora ya leo, siku ya kupokea magumu unayokutana nayo na kuyatumia kuwa imara zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania