“The younger and the more primitive a person is, the more he or she believes that life is material and that it exists only in the body. The older and wiser a person becomes, the more he or she understands that all life originates from the spirit.” – Leo Tolstoy

“I spent the first half of my life making money and the second half of my life giving it away to do the most good and the least harm.” – Andrew Carnegie

Unapokuwa kijana unasukumwa zaidi na mwili kuliko kitu kingine chochote.
Unaweka uzito kwenye kupata yale yanayohusu mwili zaidi.
Kadiri umri unavyokwenda, ndivyo unajifunza kwamba mwili hautosheki,
Unagundua kwamba roho ni muhimu na ndiyo mwongozo sahihi wa maisha yako.
Kadiri unavyolijua hili mapema, ndivyo unavyoweza kutengeneza maisha bora na tulivu kwako.
Unapojua umuhimu wa kuongozwa na roho ukiwa kijana, hupotezi muda ambao wengi wanapoteza kwenye mwili.
Haimaanishi unausahau mwili, ila unaupa uzito unaostahili na siyo kuuacha ukuendeshe na kuwa mtumwa wa mwili.

Winston Churchill amewahi kusema; ukiwa na miaka 20 unajali sana watu wanakufikiriaje, ukiwa na miaka 40 unaacha kujali watu wanakufikiriaje, ukiwa na miaka 60 unagundua hakuna hata aliyekuwa anakufikiria kama ulivyokuwa unadhani
Usemi huu unatuonesha kwamba kadiri umri unavyokwenda, tunazidi kupata hekima.
Lakini kwa maarifa yaliyopo sasa, huna haja ya kusubiri umri ndiyo upate hekima, unaweza kupata hekima na kuiishi sasa.
Iwe una miaka 20, 30, 40 au zaidi, chagua leo utayaishi maisha yenye maana kwako na siyo ya kuwafurahisha wengine, kwa sababu hakuna anayejali kuhusu wewe kama unavyodhani.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania