“Only when we forget about ourselves, when we get out of the thoughts of ourselves, can we fruitfully communicate with others, listen to them, and influence them.” – Leo Tolstoy
Kujisahau wewe mwenyewe ndiyo kuwajua wengine.
Pale unapoacha kujifikiria zaidi wewe, ndipo unapoweza kuwasiliana vizuri na wengine, kuwasikiliza vizuri na hata kuweza kuwashawishi.
Tunapoteza nafasi hizi nzuri kwa kujifikiria zaidi.
Unaongea na mtu, badala ya kusikiliza kwa makini anachosema, unafikiria utamjibu nini.
Haishangazi mawasiliano ya siku hizi yamekuwa magumu na watu hawaelewani.
Kama huwezi kuacha kujifikiria zaidi wewe mwenyewe, huwezi kumsikiliza mtu vizuri.
Kama huwezi kumsikiliza mtu vizuri huwezi kumwelewa.
Na kama huwezi kumwelewa mtu vizuri, huwezi kumshawishi.
Acha kujifikiria zaidi na anza kusikiliza zaidi.
Watu huwa wanakuambia kila unachotaka kujua,
Wanaweza wasikuambie kwa maneno, lakini wakafanya hivyo kwa matendo.
Kama umakini wako upo kwao ndiyo utaweza kuwaelewa.
Uwe na siku bora, siku ya kuacha kujifikiria zaidi wewe na kuanza kuwasikiliza wengine kwa umakini mkubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania