Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye maisha huwa kuna ukuaji wa aina mbili.

Aina ya kwanza ni ukuaji wa haraka, huu huwa unatokea kwa kipindi kifupi, mfano wakati wa balehe, mtu huwa anapata ukuaji mkubwa na wa haraka ndani ya muda mfupi.

Aina ya pili ni ukuaji wa taratibu, huu ni ule ukuaji wa kawaida ambao unachukua muda mrefu.

Sasa ukuaji wa taratibu huwa unafuatia ukuaji wa haraka ambao mtu anakuwa amepitia.

Kwenye mafanikio pia kuna ukuaji huo wa aina mbili.

Ukuaji wa haraka ambao unatengeneza msingi muhimu kwako na ukuaji wa taratibu ambao unaishi misingi uliyoitengeneza.

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha yao, kwa sababu hawajawahi kupata ukuaji wa haraka, mkubwa na wa muda mfupi kwenye eneo la mafanikio.

Na hiki ndiyo kitu ambacho programu ya GAME CHANGERS inakuletea. Inakupa nafasi ya kukua haraka kwa muda mfupi ambapo utajijengea msingi wa kuendelea na ukuaji wako.

Watu wengi wanaposikia ukuaji wa haraka, huwa hawaamini kama ni kitu kinawezekana, kwa sababu hawajawahi kujaribu.

Leo nakwenda kukushirikisha ushuhuda wa mtu aliyekuwa na wasiwasi kuhusu ukuaji wa haraka, lakini wasiwasi huo ukafutika baada ya kuweza kupitia ukuaji huo ndani ya muda mfupi wa siku 30.

Soma ushuhuda huu, kisha ukaribie kwenye programu ya GAME CHANGERS ili uweze kupata ukuaji wa haraka.

Hii ni tathmini yangu binafsi ya siku 30 za GAME CHANGERS!  Nilipata email ya kocha kama kawaida yake kutuma email za koching; neno GAME CHANGERS lilikuwa geni kwangu, japo maana yake iko wazi na inahamasisha! Laki tatu haikuwa changamoto sana kwangu; changamoto ilikuwa siku thelathini, itawezekanaje kupata badiliko? Namshukuru Mungu kwa ajili ya kocha, ni kweli ni kocha! Siku 30 nimeanzisha duka la thamani ya laki 6, kwa wiki mbili na nusu nilipata faida ya zaidi ya elfu 80, nimeweza kufungua wakala wa benki mbili na wakala wa  tigo, airtel na m mpesa, nangoja tu wanipe go ahead!

Nimeweza kuandika kitabu ambacho kitatoka mwishoni mwa mwezi wa Februari 2020! Nimeweza kuongeza marafiki wenye tija! Kutokana na programu hii nategemea mwisho wa mwaka pato langu liwe mil 50, mwakani mil 100!

Josephath Ulomi

ulomi book cover

Josephath Ulomi ni mmoja wa watu wanne walioshiriki programu ya GAME CHANGERS kwa msimu wa mwezi Januari 2020. Katika programu hii, Ulomi  alikuwa na majukumu makuu matatu, kuanzisha duka la rejareja, kuomba uwakala wa mitandao ya simu na benki na kuandika kitabu. Haya ni majukumu mengi ambayo kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuyakamilisha ndani ya siku 30.

Lakini kwa mpango bora kabisa ambayo tuliuweka pamoja, pamoja na mwongozo wa Kocha na msukumo wa washiriki wengine kwenye programu hii, Ulomi aliweza kutekeleza vizuri mipango hiyo kama alivyoshirikisha kwenye ushuhuda wake hapo juu.

Mambo hayakuwa rahisi, alikutana na vikwazo na changamoto nyingi lakini pia ana majukumu mengine makubwa sana ya kikazi na kijamii, lakini programu ya GAME CHANGERS iliweza kumsukuma kutekeleza yale aliyopanga.

SWALI MUHIMU KWAKO.

Rafiki, umeusoma ushuhuda wa mwenzetu hapo juu, ambao unatia moyo na kuhamasisha. Hapa nina swali muhimu sana kwako, je na wewe unataka kutengeneza matokeo makubwa kama hayo kwenye maisha yako ndani ya muda mfupi?

Je kuna kitu kikubwa umekuwa unapanga kufanya lakini hukianzi? Mfano kuanza biashara, kuandika kitabu, kukuza biashara au kingine chochote kwenye maisha yako?

Kama jibu ni ndiyo, kwamba unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, basi nina habari njema sana kwako. Msimu wa GAME CHANGERS PROGRAM MACHI 2020 umefunguliwa na kuna nafasi chache ambazo zimebaki.

Karibu sana ushiriki programu hii kwa mwezi Machi na upate nafasi ya kufanya makubwa sana kwenye maisha yako, ndani ya muda mfupi, ambayo hujawahi kuyafanya kabisa kwenye maisha yako.

UTARATIBU WA GAME CHANGERS.

GAME CHANGERS ni programu maalumu ya ukocha ambayo inaendeshwa na Kocha Dr Makirita Amani ambayo inawalenga wale wanaotaka kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao na kwa muda mrefu.

Programu hii inakupa manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo ni COACHING (ambapo unapata mwongozo wa kocha) na MASTER MIND (ambapo unapata msukumo wa wengine wanaofanya makubwa kama wewe). Hizi ni nguvu mbili ambazo zinakuwezesha kufanya makubwa sana zikitumika pamoja.

Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne ili kutoka pale ulipokwama sasa na kupiga hatua kubwa.

Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.

Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao. Ndani ya kundi hili kila siku kunakuwa na mijadala ya hatua ambazo kila mtu anapiga kwenye mipango aliyojiwekea kwa wiki husika.

Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.

Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.

Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.

Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.

NAFASI ZA KUSHIRIKI GAME CHANGERS MACHI 2020.

Rafiki, kama nilivyokushirikisha kwenye utangulizi, programu hii ya GAME CHANGERS huwa inaendeshwa kwa misimu, na msimu mmoja unachukua siku 30 ambazo ni mwezi mmoja.

Tunakwenda kuanza msimu mwingine wa programu hii ya GAME CHANGERS mwezi Machi 2020, kuna nafasi tano (5) pekee za kushiriki programu hii kwa msimu huo wa mwezi Machi. Hivyo karibu sana uchukue hatua sasa.

HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUSHIRIKI GAME CHANGERS.

Kama kwa kusoma hapa umeona GAME CHANGERS ni kitu unachohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa (na ni kitu unachohitaji kweli), basi chukua hatua sasa ili kuweka nafasi yako ya kushiriki programu hii.

Hatua ya kuchukua ni kutuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako na maelezo kwamba utashiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020.

Kwa kufanya hivi unajihakikishia nafasi ya kushiriki programu hii na kunufaika nayo.

Chukua hatua sasa kwa sababu nafasi zilizopo ni chache (tano pekee) na uhitaji ni mkubwa. Tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA MSIMU WA MACHI 2020.

Ada ya kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.

Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.

Msimu wa mwezi Machi wa programu hii ya GAME CHANGERS 2020 utaanza rasmi siku ya jumamosi tarehe 07/03/2020 na kumalizika siku ya jumamosi ya tarehe 04/04/2020.

Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/= kabla ya tarehe 03/03/2020. Pia tuma mapema taarifa ya ushiriki ili uweze kupata nafasi hii, kwa kutuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba utashiriki GAME CHANGERS JANUARI 2020.

Nafasi za kushiriki programu hii kwa mwezi machi ni 5 pekee, na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.

Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache chache sana.

Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020 ni tarehe 03/03/2020. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 05/03/2020 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.

Tarehe 07/03/2020 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.

Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.

Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.

Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha