“Nothing can make a person feel more noble than work. Without work, a person cannot have human dignity. It is because of this that idle people are so much concerned by the superficial, outer expression of their importance; they know that without this, other people would despise them.” – Leo Tolstoy

Hakuna kitu kinachompa mtu heshima zaidi ya kazi.
Kazi ndiyo inayokupa utu, inayowafanya wengine wakujue na kukuheshimu.
Wale wasiofanya kazi bora, hutafuta kujulikana na kuheshimika kwa mambo ya juu juu.
Lakini wewe usitumie njia hiyo, wewe tumia kazi.

Ifanye kazi yako kwa ubora wa hali ya juu sana, ifanye kwa upekee, wape watu kile ambacho hawawezi kukipata kwingine.
Wafanye watu wakujue kupitia kazi yako,
Watu wanaposikia jina lako, wanajua ni nini unafanya.

Usitake kujulikana kwa mavazi unayovaa,
Wala usitake kujulikana kwa cheo au nafasi uliyonayo,
Usitake kujulikana kwa maneno au makosa unayofanya.
Taka kujulikana kwa kazi unayofanya.

Ukawe na siku bora sana ya leom siku ya kuweka juhudi kubwa kwenye kazi yako, ili kuacha alama kwenye kile unachofanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania