“We lie to other people so often that we get used to it, and we start to lie to ourselves.” —FRANÇOIS DE LA ROCHEFOUCAULD

Kuna kichekesho kwamba mtu mmoja alienda kisimani kiteka maji, akakuta kuna foleni ndefu.
Akajiuliza nitawezaje kuchota maji kwa haraka na kuondoka? Akapata wazo, atumie uongo.
Basi akawaambia nyie mmekaa hapa wakati kuna gari la soda limeanguka kule na watu wanajichukulia soda watakavyo?
Watu waliposikia hivyo wakatoka mbio kuelekea kule walikoelekezwa.
Basi mtu yule akawa amebaki mwenyewe kisimani, akiwa na nafasi ya kuteka maji na kuondoka.
Lakini akajiuliza, mbona wameamini wote na kwenda, labda ni kweli kuma gari limeanguka, wacha na mimi niende nisije nikapitwa.

Rafiki, hilo ndiyo tatizo la kuwadanganya wengine,
Unaanza kujidanganya na wewe pia.
Kadiri wengine wanavyoamini uongo wako, ndivyo na wewe unavyoanza kuuamini, unaishia kujidanganya wewe mwenyewe.
Na hakuna kitu kibaya kama kujidanganya mwenyewe.

Mara zote simamia ukweli, sema ukweli mara zote na huwezi kujidanganya.
Utaona uhalisia na kuchukua hatua sahihi, kuliko kujidanganya na kujipa matumaini hewa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kusema ukweli na kusimamia ukweli kwenye kila jambo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania